|
|
|
![]() |
![]() |
|
|
|
||
|
Gazeti INJILI Kwenye Internet http://munishi.com Tel. 254722602445 E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com Serikali Yatatiza usafiri Kenya ![]() Kufuatia agizo la serikali kwamba matatu zote ziwekwe vithibiti mwendo pamoja na mikanda, maelfu wamekosa usafiri kwenda kwenye sehemu zao za kazi. Pamoja na kwamba matatu nyingi hazijatimiza agizo la serikali, tuna mashaka kwamba hata kama zote zitatimiza agizo hilo, matatizo ya usafiri bado yatakuwa mbali na kumalizika. Pamoja na kujaza abiria kupindukia, bado matatu zilikuwa hazikithi mahitaji ya usafiri sawa sawa. Tunaiunga mkono hatua ya serikali kushurutisha nidhamu katika sekta ya usafiri, lakini sambamba na hilo tunaitaka ichukue hatua zaidi. Hii itakuwa ni pamoja na kutengeneza barabara zilizopo pamoja na kuongeza nyingine mpya. Tena usafiri wa reli uimarishwe na ikiwezekana zijengwe reli za chini ya ardhi mijini na za kwenda mikoani. Serikali wangeanza na hilo, hili la sasa lingekuwa rahisi kutekelezeka. ILa mambo yalivyo sasa ni kwamba abiria waliotarajiwa kusaidiwa, ndio wanaoteseka na hata kuweka maisha yao hatarini zaidi. Wengi wamekosa nafasi katika matatu chache zilizotimiza agizo la serikali, na matokeo ni kupanda malori au Pick ups ambazo hazina mikanda wala vithibiti mwendo. Taxi nazo zimepata biashara kubwa ya kubeba abiria. Zenyewe hazina vithibiti mwendo wala mikanda ya kufunga. Kutokana na wingi wa abiria, nao itawabidi wakimbie mwendo wa kasi kuwahi abiria. watafanya kile kilichokuwa kinawaponza madereva wa matatu. Tamaa ya pesa. Hali kama hiyo inapotokea, abiria aliyetarajiwa kulindwa na ajali barabarani anajikuta akiwa hatarini kuliko mwanzo. Hatuipingi hatua ya serikali, lakini utekelezaji wake lazima uwe wa muda mrefu. Vinginevyo itakuwa sawa na kuruka majivu na kukanyaga moto. Matatu kama zilivyo biashara nyingine, wanataka wapate faida ili waweze kuwalipa madereva na wasaidizi wao. Inapokuwa safari ya saa moja inabidi ichukue masaa mawili hii itapunguza wingi wa safari kwa siku. Sambamba na hilo abiria waliokuwa wakijazana sasa hawatakuwepo. Ukizingatia yote hayo wenye matatu wataachwa na suluhu moja tu. Nayo ni kuongeza nauli. Siyo kwamba wataongeza, tayari wameshaongeza. Mahali pa shilingi arobaini sasa abiria wanalipa mia moja. Wakilalamika wanaulizwa kwamba "huoni umekaa raha mustarehe kuliko mwenye gari ya binafsi? Umejifunga mkanda, unasoma gazeti, kama husomi gazeti umelala usingizi, raha zote hizo hutaki kuzilipia? Hata kama ni gari yako binafsi ingebidi umwajiri dereva ndipo uweze kustarehe kama unavyostarehe hapa kwenye matatu. Na hapo hatujazungumza kuhusu petroli kila siku na matengenezo ya gari yako. Kwa hiyo wacheni maneno mengi, ongezeni nauli." Hayo ndiyo maneno ambayo abiria watakutana nayo kila watakaposafiri. Siyo kwamba matatizo ya usafiri yatawaadhiri abiria peke yao, la hasha. Hata serikali itaadhirika kwani wengi watashindwa kuwasili katika sehemu zao za kazi mapema, na hii itaharibu uchumi zaidi. Je hilo ndilo lengo la serikali? Kama jibu lake ni hapana, basi lazima marekebisho ya sekta zote yafanywe kwa makini zaidi ili wale waliotarajiwa kusaidika na marekebisho hayo wasiwe ndio wanaoumizwa nayo. Kuna mengi yanayofanywa kwa nia nzuri lakini yanageuka kuwa kero kwa wananchi. Kwa mfano majumba yanayotarajiwa kubomolewa kwa madai kwamba yamejengwa barabarani. Itaeleweka na kuingia akilini zaidi wakati ujenzi wa barabara husika utaonekana kukwamishwa na nyumba iliyojengwa kwenye mkondo wa barabara. Nyumba kama hiyo ikibomolewa itaeleweka lakini baada ya serikali kuwafidia wenye nyumba hizo. Hawa wenye nyumba hizo bado ni wananchi waaminifu kwa serikali hii mpya kama walivyokuwa waaminifu kwa serikali ya zamani iliyowamilikisha maeneo kimakosa. Ilikuwa nje ya uwezo wao kuirekebisha serikali ya awali, na hata sasa ni nje ya uwezo wao kuipinga hatua ya serikali iliyoko madarakani kubomoa nyumba zao, Pia itakuwa nje ya uwezo wao wakati serikali ijayo itakapowaruhusu wengine wajenge kwenye maeneo kama hayo. Tunayosema hapa ni kwamba serikali isiwaadhibu wananchi kwa makosa ya serikali ya awali. Serikali ya sasa inatakiwa kuiadhibu serikali ya awali na siyo wananchi. Sisi wananchi tunaiona serikali mpya kama mkombozi wetu. Ikiwa MKOMBOZI atatenda mambo yatakayowaumiza waliotarajia kukombolewa, uchungu wake utakuwa mara dufu. Kabla ya agizo
la serikali, mambo yalikuwa hivi:
|
||
|
Faustin
Munishi Tell. 25472602445 Nairobi Kenya East Africa
E-mail: fmunishi@hotmail.com | munishifaustin@yahoo.com |
||