Free Web Hosting by Netfirms
Web Hosting by Netfirms | Free Domain Names by Netfirms


Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo

Twende kanisani

Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Pastor James Maina Nganga
NENO Evangelisim Mombasa

Rev. James Maina N'gan'ga Aitikisa Mombasa.

 

Na Mwandishi wetu Mombasa

Wengi wanamwita Kunguru kwa sababu ya wimbo wake maarufu ujulikanao kwa jina hilo,wengine wanamwita nabii kwa sababu ya vipawa vyake vya kuhubiri, na kuna wale wanao wanaomjua kama muuza kanda za dini akitumia Baiskeli, bado kuna wengine wanaomkumbuka kama mfungwa wa Manyani Prison, Isitoshe kuna wale wanaomjua kama milionea anayeishi Nyali akiendesha gari ya kifaari na kuwa na kipindi kinachorushwa hewani kila wiki, na sasa yuko kwenye mtandao wa kompyuta duniani. Huyo siyo mwingine ila ni Mchungaji James Maina N'gan'ga.

Anahubiri kila siku mchana katika kiwanja cha Railway mjini Mombasa, na inasadikiwa kuwa ndiye anayeongoza kwa kuwa na kanisa kubwa mjini Mombasa au pengine Kenya. Kila jumapili huongoza ibada katika Chandaria Hall ambapo maelfu ya watu hukusanyika kila jumapili kumsikiliza Mhubiri huyu.

Lakini Rev. Maina ni nani hasa? Na ni nini kinachomfanya awe tofauti na wahubiri wengine?

Mwenyewe anasema Yesu aliyemuokoa wakati akiwa jela ndiye anayestahili sifa na utukufu wote. Yeye ni mtumishi anayetumiwa na Mungu kuhubiri neno lake ambalo ndilo linalobadilisha maisha ya watu.Ukimsikia Rev.James Maina akiongea utajiuliza maswali mengi ambayo atayajibu yote bila ya wewe kumuuliza.



Rev.James Maina N'gan'ga E-Mail: jamainga@yahoo.com Tell.25472410381


 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>