Free Web Hosting by Netfirms
Web Hosting by Netfirms | Free Domain Names by Netfirms


Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo

Twende kanisani


Ukimwi unaua: Asema Kenedy Ochieng

Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Hakuna kama Yesu Asema Farida Maria

Mwimbaji wa nyimbo za INJILI Farida Maria

"Nimejua kwa hakika kwamba hakuna kama YESU. Anasamehe wenye dhambi, anaponya magonjwa, anaokoa roho zisiende jehanamu. Ameniokoa na sasa ninamwimbia sifa na kuwahubiria wengine waujue wema wake." Hayo ni maneno ya Farida mwenyewe alipozitembelea ofisi za gazeti la INJILI River Road Nairobi hivi karibuni.


Nyimbo zake mpya za Injili zimetawala kila kituo cha redio, kila mwandishi wa habari anatamani kumhoji, na TV zote kwa sasa wana vipindi vya mahojiano naye. Pengine ni kutokana na walivyomjua Farida Malkia wa chakacha, na sasa hawaamini kama kweli ameacha kabisa kuimba kwenye vilabu vya usiku, na sasa anaimba nyimbo za injili mchana kwenye mikutano ya Injili na makanisani. Lakini kwa maneno yake mwenyewe aliliambia gazeti hili kwamba amezaliwa mara ya pili na sasa ni kiumbe kipya.


Farida akiwa na kundi lake la uimbaji wa nyimbo za INJILI

"Nikiwa safarini Dubai, mambo yangu yalianza kubadilika. Nilikosa hamu ya kufanya kile kilichokuwa kimenipeleka Dubai. Mkataba wangu wa kuimba na kucheza kwenye vilabu Dubai, karibu ungeenda mrama. Walishangaa kuniona nikiwa sifurahii tena kufanya kile walichokuwa wakingoja kwa hamu. Yaani kumba na kucheza mbele ya walevi wanaofikiri kwamba wanaifurahia dunia na uzuri wake."

Ukimsikiliza utagundua kwamba hata huko alikokuwa hawakuwa wakimchezea. Akili yake ni kama SUNGURA. Maneno mia tatu kwa dakika moja na yote yana maana.Nafikiri watapeli wa naowatapeli wanamuziki waliipata adabu yao kwa farida wakati wake.

Msikie anavyosema. "Wengine unasaini nao mkataba, lakini hawatimizi yaliyomo kwenye mkataba. Lakini tulipambana mapaka wakatulipa. Pia tulichukua hatua za tahadhari. Yaani hatufanyi onyesho kabla hatujalipwa. Hiyo ilitusaidia kama bendi."

Alianzisha bendi yake mwaka 1999 baada ya kuachana na bendi nyingine maarufu THEM MASHROOMS. Alijiunga nao mwaka1993 japo tangu mwaka 1990 ndipo alipoanza rasmi kucheza kwenye vilabu vya usiku.

Akiwa Dubai na bendi yake, ndipo hamu ya kusoma biblia ilipoanza. Hakujua kwa nini, lakini moyoni alisikia sauti ikimwambia atubu dhambi kwani maisha yake kiroho hayakuwa mazuri. Hali hiyo ilimsumbua mpaka alipomaliza mkataba wake huko. Kutokana na mabishano moyoni, wengi walimuona Farida waliyemzoea kama anabadilika polepole kuwaacha. Alipenda kuomba na kuwahimiza wanabendi waombe Mungu. Hakuwa na amani moyoni, jambo lililopelekea kutafuta kanisa aombewe.

Alimkumbuka Mchungaji aliyekuwa amemuombea dada yake aliyekuwa na Kansa na akapona mara moja, na akaona aende kwake. Pamoja na kwamba yeye mwenyewe aliwahi kuombewa na mchungaji huyo huyo na kupona kabisa vidonda vya tumbo, lakini alimkumbuka zaidi kwa kumponya dada yake. Alipomwendea, alimwambia amponye na roho yake kama alivyofanya. Kwake mchungaji ndiye aliyekuwa akiponya. Mchungaji alimpokea na kumfundisha kwamba YESU ndiye anayeponya na wala siyo yeye. Alimtaka amwamini Yesu na kutubu dhambi. Baada ya maombi,anasema mwenyewe kwamba aliokoka.

Msikie." Sasa nimezaliwa mara ya pili. Nimeokoka na nimejua hakika ya kwamba HAKUNA KAMA YESU." alizaliwa mwaka 1970 huko machakos. alisomea katika shule ya msingi EDALVALE na baadaye KENEDY HIGH SCHOOL. Pia alipata mafunzo ya usekratari, lakini kabla hajaanza kazi, alianza kcheza kwenye vilabu vya usiku.

Sikumjua enzi zake, lakini sasa anaonekana kwenye rinda ndefu, nywele zake ni ndefu zinazoweza kuufunika uso, hana mapambo mengi usoni, na kila siku yuko bize kusambaza kaseti na CD yake madukani pamoja na kuimba kwenye mikutano ya Injili. Hajaolewa, na anasema hilo siyo suala kwa sasa.

" Kwa sasa suala ni kuijua biblia vizuri kama nilivyoijua KORANI, halafu nimtumikie Mungu vilivyo. Mengine ya mume baadaye. Najua Mungu hawezi kunichagulia, kazi hiyo nitaifanya mwenyewe. Lakini nitachagua katika wale atakaowaleta mbele yangu." Alimaliza Farida Maria.


 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>